Header Ads

Zilizotufikia Punde

Video: Wasanii watua nyumbani kwa RC Makonda, RC atoa ahadi hii kuhusu Roma





Kamanda wa polisi kanda maalum ya Dar es Salaam, Simon Sirro, Jumamosi hii atakutana na wasanii kuwaeleza taarifa ya jeshi hilo kuhusiana na kupotea kwa rapper Roma Mkatoliki na wengine waliotekwa na watu wasiojulikana usiku wa Jumatano katika studio za Tongwe Records.
Katika mkutano na waandishi wa habari Ijumaa hii, Katibu Mkuu wa chama cha wasanii wa kizazi kipya, TUMA, Samweli Andrew Mbwana maarufu kama Brighton amesema amefanikiwa kuongea na Kamanda Sirro Ijumaa hii.
“Yeye [Sirro] ametusisitiza kwamba tuendelee kuwa na uvumilivu hili suala wao wanalishughulikia, na bahati nzuri wao kama polisi wameshapata taarifa zetu, wameshafungua jalada,” amesema Brighton.

“Simon Sirro ametuhakikishia hilo, yuko na chombo, ameunda chombo maalum katika kuhakikisha kwamba hawa ndugu zetu wanapatikana salama. Na vile vile ametuahidi kesho saa tano na nusu wote kwa umoja wetu, wasanii pamoja na ndugu zetu waandishi wa habari tufike ofisini kwake pale ataweza kutupa taarifa ya hali inavyokwenda na wapi amefikia kama amewapata ama kuna taarifa yoyote kuhusu wao ambao wamepotea,” ameongeza.

Brighton ameiomba jamii kuwaunga mkono wasanii hao kuhakikisha Roma na wenzake wanapatikana wakiwa salama. Wengine waliopotea ni rapper Moni Centrozone, producer wa Tongwe Bin Laden wengine watatu

WATCH VIDEO

 

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda, wameahidi Roma Mkatoliki, Moni pamoja na wengine wawili kupatikana Jumapili hii baada ya wasanii hao kutekwa na watu wasiojulikana Jumatano hii wakiwa 

Tongwe Record. Alisema hayo akiwa nyumbani kwake Masaki jijini Dar es salaam, muda mchache baada ya kutembelewa na wasanii ambao walimtaka mkuu huyo kuwasaidia kupatikana kwa wasanii hao. Akiongea na waandishi mbele ya wasanii hao, RC Makonda alisema kila mtanzania ana nafasi ya kumtafuta Roma na wenzake kwa kuwa hakuna anayejua watu hao wako wapi. “Natoa pole kwa ndugu pamoja na marafiki, hakuna mtu ambaye anaweza kupotelewa na mtu akawa na furaha na bahati mbaya tunaangaika kujua wapi waliko. Nitumie fursa hii kuwaambia wananchi wa mkoa wa Dar es salaam kwamba tunapopotelewa na ndugu zetu katika mazingira ambayo hatuyafahamu sio wakati ya kuyarusha rusha maneno na kufika hatua tunapoteza ushahidi,” alisema RC Makonda. Alisema tayari ameliagiza jeshi la polisi kufuatia suala hilo kwa ukaribu zaidi ili kupata ufumbuzi mapema huku akiahidi mpaka Jumapili hii watu wao watakuwa wamepatikana.

 

No comments