“Kesho Ibada itakuwa LIVE on YOUTUBE kuanzia saa nne na nusu, kutoka Kanisa la Ufufuo na Uzima, Ubungo Kibo Dar es Salaam. Usikose.,” aliandika Gwajima Instagram akiambatanisha na picha (hapo juu Baada ya ujumbe huo wa Gwajima, Diamond amerudi upya kuomba radhi kuhusu kumhusisha mchungaji huyo kwenye wimbo wake.
“Yala! Yala! Jamani Mwenzenu nimeyatimba….. lakini mi nafkiri watu wanatakiwa waiskilize hii nyimbo kwa umakini sana tena sana na wataelewa nini ilikuwa maana yangu haswa… Hususani kama kipengele nilichomtaja mzee wangu @Bishopgwajima nilisema: “mara nasikia vya aibu Konda na Gwajima eti ugomvi umekolea….ila kuchunguza kwa karibu ni kuna binti mmoja tu ndio kwa mitandao anachochea…” Point yangu ni kwamba licha ya kweli kuna yaliyojiri nyuma, lakini kwa busara zao ninazoamini wamejaaliwa na Mwenyez Mungu muda si mref wangekaa chini na kumaliza…nawote kufurahi kwa pamoja, lakini kwakuwa kuna dada mwingine alikua anachochea hawa ndugu zetu wazidi kufarakana…ikapelekea hadi kufikia hapa…asa hapo kosa langu mie liko wapi? Chonde chonde mzee wangu @Bishopgwajima usinigeuze maji kesho , mana nakujua ukimuamulia mtu…. naweza jumapili ya kesho nikaiona chungu Mwaka mzim,” aliandika Diamond Instagram. |
No comments